January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Bunge la Tanzania ajiuzulu

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spread the love

 

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amejizulu nafasi hiyo leo Alhamisi 6 Januari 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ndugai ameandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nakala kuiwasilisha kwa katibu wa Bunge.

Amechukua uamuzi huo baada ya kuwapo kwamashinikizo kutoka kila pande hususan CCM kumtaka kujiuzulu kutokana na kupinga mikopo ya serikali.

Tayari Ofisi ya Bunge nayo imetoa taarifa kueleza kuwa imepokea barua ya katibu mkuu wa CCM ikieleza nafasi ya spika iko wazi na utaratibu wa kuijaza utatangazwa baadaye.

error: Content is protected !!