Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaji, Hakimu Zanzibar wapewa kibarua
Habari Mchanganyiko

Majaji, Hakimu Zanzibar wapewa kibarua

Spread the love

 

MAJAJI wa Mahakama Kuu Zanzibar na mahakimu visiwani humo, wameombwa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, kupitia nafasi zao kwenye mhimili huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Wito huo umetolewa katika semina ya siku mbili, tarehe 27 na 28 Novemba 2021, ya kuwakumbusha namna ya kushughulika na mashauri ya haki za binadamu, iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Hamis Ramadhan, amewataka majaji na mahakimu kushughulikia kwa wakati kesi za udhalilishaji wanawake na watoto, ili kutokomea vitendo hivyo.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za udhalilishaji wanawake na watoto hapa Zanzibar, mafunzo haya yatusaidie kuona umuhimu wa kushughulikia mambo haya,” amesema Jaji Ramadhan.

Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Hamis Ramadhan

Naye Kamishna kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Zanzibar, Khatib Mwinyi Chande, amesema mahakama ni taasisi inayopaswa kuisaidia Serikali kutatua matatizo ya wananchi wake.

“Kufungua mashauri mahakamani ni namna pekee ya kutetea na kukomesha uvunjaji wa aina yoyote wa haki za binadamu ambazo ni za muhimu kwa kila mtu. Mahakama ni taasisi zinazopaswa kuisaidia Serikali kutatua matatizo hayo na si vinginevyo,” amesema Chande.

Kamishna wa THBUB-Zanzibar, Khatib Mwinyi Chande

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema mtandao huo umeandaa mafunzo hayo kwa majaji na mahakimu, ili kuwakumbusha umuhimu wao katika mashauri yanayohusiana na haki za binadamu.

“Tunatambua kuwa majaji na mahakimu ni watetezi muhimu wa haki za binadamu, tuitaendelea kuwa na utaratibu huu wa mafunzo ili kukumbushana wajibu wetu,” amesema Olengurumwa.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!