Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia asisitiza utafiti chanzo kanda ya ziwa kuongoza kwa saratani
Habari za Siasa

Rais Samia asisitiza utafiti chanzo kanda ya ziwa kuongoza kwa saratani

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto na Walemavu kushirikiana na Hospitali ya Kanda ya Ziwa ya Rufaa Bugando kubaini sababu za kuenea kwa saratani kanda ya ziwa hususani kwa wanawake ambayo imezidi kuenea kwa kiasi kikubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia ameuagiza uongozi wa Hospiali hiyo ya Bugando, kutumia vema mgawo wa fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambapo hospitali hiyo itapewa Sh bilioni 4.2.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Novemba, 2021 wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando jijini Mwanza.

Akizungumzia kuhusu mradi wa jengo la huduma za saratani, amesema maelekezo ya mtangulizi wake (Hayati Rais Dk. John Magufuli) ni kwamba wizara ya afya kuhakikisha wanashirikiana hospitali hiyo kufanya tafiti na kubaini sababu za kuwa na kiwango kikubwa cha sarakati katika kanda ya ziwa.

“Ni jambo la kusikitisha kuona idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani inakua ndani ya kanda ya ziwa kwa mfano kwa mwaka 2019 mlipokea wagonjwa wapya 1200, ambao walihamasika kuja kupima na kwa mwaka 2021 mnaweza kufikia wagonjwa 1500.

“Hii ni idadi kubwa sana kwa magonjwa haya, nielekeza umuhimu wa tafiti kujikita zaidi kwenye kubaini chanzo cha saratani hizo na kwanini kanda ya ziwa inaongoza kwa wahanga wa saratani ambapo wanawake ndio wahanga wakubwa wa saratani za kizazi na matiti,” amesema.

Amesema kuna sababu kadhaa zinatolewa, ikiwamo uchafuzi wa mazingira kutokana na uchimbaji na matumizi zebaki.

“Wakati wanafanya nuchimbaji na uchekechaji wa madini kwenye mito na hutumia zebaki, maji yakisambaa watu wa baadhi ya maeneo wanakunywa.

“Saratani inaenea kwa watu lakini kubwa inaonesha ni wanawake, hapa ndipo inapoleta swali kwanini?. Kama ni zebaki ingekuwa kwa wote.

“Kwa hiyo nitie shime katika kuendeleza tafiti hizi na tubaini ni kwanini ili tuweze kuchukua hatua na tupunguze balaa hili linalotuzonga,” amesema.

Akizungumzia kuhusu fedha hizo za IMF, Rais Samia amesisitiza kuzingatia ubora wa vifaa vya matibabu hata kama taratibu za manunuzi zinavunjwa ili kuendana na muda wa matumizi wa fedha hizo ambao ni miezi tisa.

Awali Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Dk. Fabian Massaga amesema hospitali hiyo ina vitanda 950 na wafanyakazi 1800 kati ya 2554 wanaohitajika.

“Kati ya wafanyakazi waliopo, jumla ya wafanyakazi 1,191 sawa na asilimia 66 wanalipwa mshahara na serikali na waliopo wanalipwa mshahara kutokana na makusanyo ya ndani ya taasisi.

“Hospitali inahudumia zaidi wananchi milioni 18 katika mikoa nane; Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora na Kigoma pia tunahudumia wananchi kutoka nchi jirani kama Uganda, Kenya, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

“Kwa wastani hospitali inahudumia wagonjwa 1400 kwa siku hii ni idadi kubwa ikilinganishwa na hospitali nyingine na ukizingatia inamiaka 50 tangu ilipoanzishwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!