December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TCRA, TUZ wakutana Dar

Spread the love

 

WAJUMBE wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) wametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wajumbe ho wamepokelewa na viongozi mbalimbali wa TCRA, akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Dk. Jabiri Bakari ambaye na kuwaeleza jinsi mamlaka hiyo inavyofanya kazi zake.
Katika ziara hiyo, TCRA na TUZ wameashiria nia ya kuhuisha baadhi ya vipengele vya mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili kwa lengo la kuboresha huduma wanazosimamia.

Pia, wamepata ufafanuzi juu ya mfumo wa ugawaji na usimamizi wa masafa, utangazaji na utoaji wa leseni za mawasiliano

TUZ imeweka bayana dhamira yake ya kuboresha zaidi huduma zake mara baada ya ziara hiyo ya mafunzo ikiwemo utoaji huduma za mawasiliano pamoja na maandalizi ya kupokea mabadiliko ya TEHAMA katika kuboresha sekta ya mawasiliano Zanzibar.

error: Content is protected !!