Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Michezo Super Sunday: Vigogo Ulaya kutifuana
Michezo

Super Sunday: Vigogo Ulaya kutifuana

Spread the love

 

NI sikukuu ya wapenda soka. Siku kubwa na yenye mvuto wa aina yake ulimwenguni. Ndivyo unaweza kuielezea leo Jumapili, tarehe 24 Oktoba 2021, maarufu ‘Super Sunday. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Miamba ya soka ulimwenguni, inakutana katika michezo ya ligi kuu za nchi yao, Seria A- Italia, La Liga- Hispani, EPL- Uingereza, Ligue 1- Ufaransa na Ereddivisie nchini Uholanzi.

Kuanzia saa 11:15 jioni, nyasi za Camp Nou, zitashuhudia shughuli ya wanaume wawili nchini Hispania wenye uhasimu mkubwa, Barcelona wakipepetana na Real Madrid.

Utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Barcelona kuumana na Real Madrid pasina uwepo wa nahodha wake, Lione Messi ambaye ametimkia Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa.

Huko Ufaransa, Messi atakuwa na kazi ya kuwaongoza mastaa wenzake kama Neymar na Mbape kuwavaa Marseille kuanzia saa 3:45 usiku.

Marseille, itakuwa nyumbani katika uwanja wake wa Stade Orange Velodrome, ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi 17 kati ya michezo tisa iliyocheza huku PSG ikiongoza ligi hiyo kwa pointi 27 kati ya michezo kumi.

Lens inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 18, kati ya michezo 10 iliyocheza.

Nchini Uingereza, majogoo wa Liverpool, watasafiri kwenda Old Trafford kuwavaa Manchester United inayoshika nafasi ya sita ikiwa na pointi 14 kati ya michezo nane huku Liverpool ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 18, baada ya kucheza michezo nane.

Utamu na ugumu wa mchezo huo ni baada ya hamasa ambayo Man U inayonolewa na Ole Gunnar Solskjaer kuwa na mshambuliaji mkongwe na mahari Cristiano Ronaldo huku Liverpool ikiwategemea Mohamed Salah kwenye mchezo huo utakaoanza saa 12:30 jioni.

Seria A, katika dimba la Giuseppe Meazza linalotumiwa na Inter Milan itashuhudia wakiwaalika kibibi kizee cha Turin, Juventus kwenye mchezo utakaoanza 3:45 usiku.

Inter iliyoshuka uwanjani mara nane, inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 17 huku Juventus iliyocheza michezo sawa na Inter inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 14 huku vinara wa ligi hiyo mpaka sasa ni AC Milan yenye pointi 25 ikiwa imecheza mechi 10.

Kudhihirisha ni jumapili kubwa, huku Uholanzi miamba ya soka nchini humo Ajax itawaalika PSV Eindhoven ambao kwa pamoja mpaka sasa wamecheza michezo tisa. Ajax inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja, ikiwa na 22 huku PSV ikiwa na 21.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!