Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Bilioni 2 kuboresha pori la Swagaswaga Dodoma, Dk. Ndumbaro atoa neno
Tangulizi

Bilioni 2 kuboresha pori la Swagaswaga Dodoma, Dk. Ndumbaro atoa neno

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imetenga Sh.2 bilioni kwa ajili ya kutengeneza bango na geti la kuingilia kwenye Pori la Akiba la Swagaswa lililoko wilaya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Fedha hizo zitazotumika kutengeneza kituo cha taarifa ya watalii na eneo la mapumziko ya watalii wakati wa kusubiri huduma ili kiwe kitovu cha utalii na kinachovutia.

Pia, serikali imesema licha ya hifadhi hiyo kubakiza hatua moja kuwa hifadhi ya taifa, mpango wao ni kuibakiza kuwa pori Tengefu.

Hayo yamesemwa jana Jumamosi, tarehe 23 Oktoba 2021 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro wakati akizindua Miradi ya Saba ya maendeleo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Miridi ya pori la akiba Swagaswaga ni pamoja na Jengo la ofisi za wahifadhi wa wanyamapori, hosteli ya mapumziko kwa wageni na watalii, nyumba za kuishi za wahifadhi na kisima cha maji chenye urefu wa mita 100 kwenda chini kinacho pampu za kisasa.

Alisema wanataka kulifanya pori hilo la Swagaswaga linakuwa kitovu cha Utalii kwa mkoa wa Dodoma na viunga vyake na watahakikisha kinaleta manufaa makubwa kwa Taifa kwa kuingiza fedha za kigeni kupitia watalii.

“Pori hili sisi hatutaki liwe hifadhi ya taifa, tunataka liendelee kuwa pori la akiba, tumetenga kiasi cha Sh.2 bilioni kwaajili ya kujenga lango la kuingilia kwenye hifadhii hii litakolikuwa na ambo mengi ikiwemo taarifa ya huduma za utalii,” alisema Dk. Ndumbaro

“Watu wanaoishi Dodoma siku za Jumamosi na Jumapil watahamia Swagaswaga kuangalia vivutio vya utalii, mji wa kwa mtoro tutaubadilisha, ni wakati sasa wa kupima maeneo yanaoyopakana na hifadhi ili kutenga maeneo ya uwekezaji na uhifadhi,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alisema licha ya miradi hiyo ambayo mamlaka imeweza kutekeleza tayari wamepata fedha kiasi cha Sh.12 bilioni na bodi itahakikisha fedha hizo zinatumika vizuri bila upotevu wowote ule.

Kuhusu hosteli iliyojengeka amesema ina vyumba 18 hivyo lazima kuwe na maeneo ya uwekezaji wa hole na makambi ya utalii.

Dk.Ndumbaro aliagiza serikali ya kijiji kutenga maeneo ya uwekezaji na kwamba serikali itawasaidia kuyatakangaza kwa wakezaji ili waweze kufika na kuwekeza kwa kujenga vivutio vya utalii ikiwa ni pamoja na hoteli za kulala wageni.

“Suala la uifadhi lina umuhimu mkubwa kwani kuna baadhi ya watu wanaaamini swagaswaga ni mali ya wizara si hivyo hii ni mali ya watanzania wote, Hivyo maeneo yanayozunguka hifadhi ni lazima wayalinde kwa juhudi zote wasifanye uharibifu kwa kuchoma mikaa na kukata miti hivyo.

“Maeneo haya yana umuhimu mkubwa sana hivyo jukumu la kuyatunza ni letu sote, nimesikia kuna wananchi wanamgogoro wa ardhi hili sio sawa kaangalieni nyaraka za pori la swagaswaga lilianza lini na nyaraka ziatasema,” alisema

Waziri huyo alifafanua kuna watu kazi yao ni kutengeneza migogoro lakini wanatakiwa kutambua kuwa kwa kwa sasa migogoro yote itathibitiwa kwa kuwa nyaraka zinaongea uhalisia wa mambo na kupitia hizo inakuwa ni rahisi kutatua migogoro yote itakayojitokeza.

Akizungumzia changamoto ya miundombinu ya barabara na amewahakikishia wananchi kuwa wataishughulikia kwa kuomba fedha maalumu kwaajili ya barabara hiyo na serikali inafikiria kuijenga barabara kwa kiwango cha lami ili watalii waweze kupita kwa uraisi.

Dk. Ndumbaro aliwahasa wananchi kuacha vitendo vya ujangili badala yake washilikiane na TAWA ili miradi mikubwa kama inayoendelea kutekelezwa ilindwe.

Hata hivyo alisema serikali haitaweza kuwavumilia watu ambao watahusika na masuala la ujangili kwani ni jambo baya.

Katika hatua nyingine, waziri aliiongezea muda bodi hadi itakapotagwazwa tena kwasababu inafanya kazi nzuri.

“Nakuagiza mwenyekiti wa bodi tuletee propozo ya kuifungua swagaswaga, barabara na hosteli nyingine ili tuwaletee fedha haraka sana tunataka swagaswaga ibadilike,”ameelekeza.

Akizungumzia agenda za nchi, Dk.Ndumbaro alisema nchi ina agenda zake, ambapo agenda ya kwanza ni chanjo ya covidi 19,wananchi chanjeni na kusikiliza maelekezo ya watalaam wa Afya.

Wananchi wote, askari wote wa wanyamapori nawasii licha ya kuwa chanjo ni hiari, lakini mkachanje ili mjiweke salama kwa afya zenu.

Agenda nyingine ni Sensa ya watu na makazi toeni ushirikiano ili tupate majibu sahihi na tunapojenga miundombinu tujue tunahudumia watu wangapi, hivyo mwakani mjitokeze na mhamasishane kwawingi ili tupate sense sahii,”alisisitiza.

Kamishina wa uhifadhi Swagaswaga, Mabula Nyanda akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo Saba alisema Pori hilo lilikuwa sehemu ya uwindaji,na baada ya makao makuu kuahamia Dodoma na lilibadilishwa na kuwa pori la akiba la utalii wa picha.

“Tunaamini mtapata wageni wengi zaidi ujenzi huu ambao umefanyika ni fahari kubwa kwa bodi kwakuwa inaacha alama kubwa kwa kufanya marekebisho,” alisema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya (TAWA), Meja jenerali Mstafu, Hamis Semfuko alieleza jinsi gani bodi ilivyojipanga kuchimba visima kwenye vijiji vinavyozunguka mapori ya akiba ili kuondoa tatizo la maji huku akimhakikishia Waziri kuwa wataendelea kufanya kazi nzuri iliyotukuka katika kipindi chote alichowaongezea muda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!