November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Geita waishiwa uvumilivu, wamtimua Ndayilagije

Spread the love

 

Klabu ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha wa kikosi hiko Ettiene Ndayilagije, mara baada ya kushindwa kutimiza malengo waliokubaliana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ndayilagije amekuwa kocha wa kwanza kutimuliwa, toka kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22.

Taarifa ya kufungashiwa virago kocha huyo, imetolewa na uongozi wa timu hiyo, mara baada ya kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika michezo minne waliocheza mpaka sasa, Geita Gold ambayo ilikuwa chini ya Ndayilagije imeambulia jumla ya pointi mbili.

Geita ilianza kupoteza mchezo dhidi ya Namungo FC mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0, kisha akapoteza tena mchezo mwengine dhidi ya Yanga, kwa bao 1-0.

Maamuzi ya kumtimua kocha huyo yalikuja mara baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1, dhidi ya Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani.

Ndayilagije amedumu miezi miwili tu, toka alipotambulishwa kama kocha mkuu wa kikosi hiko tarehe 22 Agosti, 2021

error: Content is protected !!