Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Rais Samia: Uchaguzi mkuu 2020 ulifanyika vizuri sana
Tangulizi

Rais Samia: Uchaguzi mkuu 2020 ulifanyika vizuri sana

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2020 akisema “ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo ameyasema leo Jumamosi, tarehe 21 Agosti 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akipokea ripoti ya uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na urais uliofanyika Jumatano ya 28 Oktoba 2020.

Rais Samia amewapongeza Watanzania kwa kushiriki kikamilifu kuanzia zoezi la uandikishaji, kupiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu huo ambao chama chake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mshindi wa urais na kuzoea karibu majimbo na kata zote.

“Hakuna shaka, yeyote aliyeshuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka jana alishuhudia jinsi ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana,” amesema Rais Samia.

“Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi mkuu mwaka 2020 kuna changamoto. Na hii ndiyo sababu ya kuandaliwa kwa ripoti ili kutoa fursa kwa wadau kuichambua na kutoa mapendekezo ili kuboresha chaguzi zijazo,” amesema.

Amiri Jeshi Mkuu huyo amesema “tuombe uchaguzi ujao uwe bora na mzuri zaidi kulingana na mapendekezo ya tume.”

“Shukuran zangu kwa vyama vya siasa kwa kujitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita na hususan chama changu cha CCM kwa ushindi mkubwa na tunawashukuru wale ambao hawakutupigia kura kwani walitekeleza wajibu huo na hiyo ndiyo demokraisa,” amesema Rais Samia.

Hayati John Magufuli

 

Katika uchaguzi mkuu huo, Rais Samia alikuwa mgombea mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuibuka na kutangazwa mshindi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Dk. Magufuli aliapishwa tarehe 5 Novemba 2020 kuwa Rais na Samia kuwa makamu wa Rais kumalizia ungwe ya miaka mitano. Hata hivyo, Rais Samia alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 na nafasi yake akaapishwa Samia kuwa Rais.

Aidha, katika makabidhiano hayo ya ripoti, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na baadhi ya vyama vya siasa huku vyama vine vikisusia shughuli hiyo.

Vyama hivyo vyenye nguvu vilivyosusia ni Chadema, NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo na CUF vikiwa na madai kwamba, uchaguzi huo uliopita haukiwa hura na haki hivyo haviwezi kushiriki hafla hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!