Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Michezo Babu Tale aweka V8: Twaha Kiduku Vs Mwakinyo
MichezoTangulizi

Babu Tale aweka V8: Twaha Kiduku Vs Mwakinyo

Gari aina ya Toyota Land cruiser V8
Spread the love

 

SHAUKU ya Watanzania kuwashuhudia mabondi wenye viwango vya juu kwa sasa nchini humo, Twaha Rubaha maarufu ‘Twaha Kiduku’ na Hassan Mwakinyo wakipanda ulingo, linaweza kufikiwa baada ya Gari jipya aina ya V8 ya mwaka 2020 kuwekwa mezani ili “wazichape.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Gari hilo linalofikia thamani ya zaidi ya Sh.200 milioni, likiwa limelipiwa kodi, limetangazwa kutolewa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Hamis Taletale maarufu Babu Tale.

Babu Tale ametangaza kutoa gari hilo baada ya Twaha Kiduku anayetokea Morogoro kuibuka mshindi dhidi ya Abdallah Pazi maarufu Dulla Mbabe kwenye pambano lililopewa jina la ‘Payback.’

Pambano hilo la raundi 10, lililofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi tarehe 21 Agosti 2021 lilishuhudia Twaha Kiduku akimpiga kwa pointi mshindani wake Dulla Mbabe.

Twaha Kiduku

Katika pambano hilo, lilishuhudiwa Kiduku akidondoshwa raundi ya kwanza baada ya kupigwa konde na Dulla Mbabe ambalo alishindwa kuhimili na baada ya kurejea raundi zingine, Dulla alipelekewa masumbwi mfululizo.

Ushindi huo, ulimfanya Twaha Kiduku kuwa mbabe wa Dulla baada ya kumpiga mara mbili katika mapambano matatu waliyokwisha kucheza huku moja walitoka sare.

Twaha Kiduku ameondoka na gari jipya aina ya Crown.

Baada ya ushindi huo, Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu nchini Tanzania, Diamond Platinum amemweleza mbunge wenzake wa CCM jimbo la Muhenza mkoani Tanga, Hamis Mwinjuma maarufu ‘Mwana FA’ amshauri Hassan Mwakinyo akubali pambano na Twaha Kiduku.

Hassan Mwakinyo

Babu Tale ni mbunge wa kutoka Mkoa wa Morogoro anakoishi Twaha Kiduku na Mwana FA ni wa Tanga ambako anatoka Hassan Mwakinyo.

“Wapeni salaam Morogoro ndio mkoa pekee unaobeba magari yenu yooote ya Dar.. Tanga eeeh kubalini basi tumalize hili jambo,naweka V8 ya mwaka 2020… Oya @mwanafa mjuze mwanao basi. Asante @twaha_kidukuumetuheshimisha wana Morogoro,” ameandika Babu Tale.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

error: Content is protected !!