May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Tuliwashughulikia tukapita bila kupigwa

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM

Spread the love

 

MWENYEKITI wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameshauri marekebisho ya sheria ili mtu anayekosea herufi ya jina lake au chama asienguliwe kushiriki uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amesema hayo leo Jumamosi tarehe 21 Agosti 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 wa madiwani, wabunge na urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mwenyekiti huyo wa CCM amepokea mapendekezo ya tume hiyo ya kuziaunganisha baadhi ya sheria ili uchaguzi mkuu na ule wa serikali za mitaa zisimamiwe na chombo kimoja hivyo akawaomba wadau kulijadili na serikali itaona njia bora ya kulifanyia kazi.

Kingine alichozungumzia ni kuenguliwa kwa wagombea wa udiwani na ubunge kwa makosa ya ujazaji wa fomu akisema “kuziangalia sheria zetu ili zisitumike kuwanyima watu haki kiufundi mathalkani mtu anaposhindwa kuandika herufi ya jina lake au chaka chake.”

Kauli hiyo imewafanya washiriki wa halfa hiyo hususan vyama kushangilia huku Rais Samia akisema “nilijua mtashangilia hili kwani tuliwashughulikia sana na kutuwezesha kupita bila kupigwa.”

Eneo jingine ambalo Rais Samia amesema, ni wadau wakae na kuangalia mapendekezo yaliyotolewa ya kuunganisha sheria ili uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa kusimamiwa chombo kimoja akiwataka wadau kujadilia na kisha Serikali itaona jinsi kipi kifanyike.

“Pendekezo naliona ngumu ni kuwa na wasimamizi wa kudumu mpaka ngazi ya halmashauri, itasababisha kuwa bajeti kubwa sana,” amesema.

Rais Samia ametumia fursa hiyo kuviasa vyama vya siasa kutoa nafasi kwa wanawake ambao ni chachu ya maendeleo.

“Nazihimiza asasi za kiraia ili kutoa elimu ya ushiriki wa wanawake katika chaguzi. Lakini nawahimiza vyama vya siasa kuwaamini wanawake na kuwateua katika nafasi za uongozi,” amesema.

Akisisitiza hilo, Rais Samia amesema “wanawake wenyewe kujiamini na kujitokeza kugombea. Natoa rai kwa vyama vya siasa kuwaamini wanawake na kuwapa fursa za uongozi. Nchi yetu haiwezi kusonga mbele kama nusu ya wanawake watabaki nyuma.”

Shughuli hiyo imesusiwa na vyama vikuu vinne nchini Tanzania vyenye nguvu ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo. Vimetoa sababu kwamba, uchaguzi huo ulikithiri ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za uchahuzi.

Vyama hivyo vimedai, kushiriki kwenye shughuli hiyo ni kuhalalisha makossa yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na washirika wake. Hata hivyo, NEC imekuwa ikisisitiza uchaguzi ulikuwa huru na haki licha ya uwepo wa changamoto ndogondogo.

error: Content is protected !!