Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Gwajima aipa siku 10 MOI
Afya

Dk. Gwajima aipa siku 10 MOI

Spread the love

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, ametoa siku 10 kwa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), iwasilishe changamoto zake, kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaa…(endelea).

Dk. Gwajima alitoa maelekezo hayo jana tarehe 17 Julai 2021, alipozungumza na uongozi wa MOI, jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo wa afya alitoa maelekezo hayo, baada kubaini taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zinazoikwamisha kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha, Dk. Gwajima ameipongeza MOI kwa kendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania, kwa zaidi ya miaka 25 tangu ilipoanzishwa.

“ Hongereni mnafanya kazi nzuri, nimekuja hapa tujadiliane ili tuone ni namna gani MOI itafikisha miaka 30 ikiwa bora Zaidi, kueni huru kuchangia mada ili tusonge mbele Zaidi.” Alisema Dk. Gwajima

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI, Prof. Charles Mkonyi, alisema hiyo ina mpango wa kuanzisha kliniki katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, ili wananchi wapate huduma.

“Pamoja na kuanzisha hizi kliniki, pia tunalenga kujenga hospitali ya kisasa ya utengamano, katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Mpiji jiji Dar es. Salaam, Alisema Prof. Mkonyi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa MOI, Dk. Respicious Boniface alisema taasisi hiyo imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi wa mikoani, ili kuwapunguzia adha ya kusafiri kufuata huduma Dar es Salaam.

“Tumesogeza huduma za kibingwa za ubongo KCMC pamoja na Bugando tumesogeza huduma za Mifupa, Hospiali ya kanda Mbeya na Nyangao Lindi Alisema Dk. Boniface.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!