Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba kusaka rekodi mpya mbele ya Kaizer Chiefs
Michezo

Simba kusaka rekodi mpya mbele ya Kaizer Chiefs

Spread the love

 

KIKOSI cha Simba kesho kitashuka dimbani kuwakabili Kaizer Chiefs kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika huku wakiwa na matamanio ya kuweka rekodi ya kucheza tena nusu fainali kama walivyofanya mwaka 1974. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Simba itaweza kusonga mbele kwenye hatua hiyo kama itapata matokeo mazuri kesho  kwa kupata ushindi au sare yoyote kabla ya kuja kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Tarehe 22 Mei, 2021.

Kwenye nusu fainali hiyo ya mwisho mwaka 1974 ambayo Simba walicheza walicheza na klabu ya Ghaz El Mahalla kutoka nchini Misri na kutolewa kwa jumla ya penati 3-1, mara baada ya kufungana bao 1-1, kwenye michezo yote miwili.

Kama watafanikiwa kufuzu kwenye hatua hiyo wataweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla kucheza nusu fainali mara mbili kwenye michuano hiyo.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamesafiri kwenda Afrika Kusini wakiwa na wachezaji 25 huku malengo yao makubwa yakiwa ni kuibuka na matokeo mazuri ili kucheza tena nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili toka miaka 47 kupita.

Kikosi cha Simba

Kwenye msimu wa 2019 Simba iliishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mara baada ya kutolewa na klabu ya TP Mazembe kwa jumla ya mabao 4-1, katika michezo yote miwili.

Kwa sasa Simba imeaimalika kwenye michuano hiyo toka alipokuja kocha Didier Gomes ambaye aliiongoza timu hiyo kwenye michezo sita ya hatua ya makundi na kumaliza kinara wakiwa na pointi 13 mbele ya mabingwa watetezi klabu ya Al Ahly, AS Vita na El Merreikh.

Wakati wakiwa safarini kuelekea nchini Afrika kusini Gomes alikuliwa akisema kuwa wanaenda kucheza mchezo huo mgumu huku wakiwa na malengo ya ushindi ili kila mtanzania na washabiki wa Simba wajivunie timu hiyo.

“Tunafuraha kucheza huo mchezo tumeusubiri kwa muda mrefu na itakuwa mechi ngumu, tutacheza kwa tahadhari na kujitolea,  tunataka kuwafanya watanzania na mashabiki wa simba kujivunia.” Alisema Didier

Simba inashuka Dimbani huku ikiwa na rekodi nzuri kwenye michezo ya ugenini kwenye hatua ya makundi ambapo katika michezo mitatu waliocheza wameruhu bao 1 dhidi ya Al Ahly na pia kuibuka na ushindi ugenini dhidi ya AS Vita na kwenda sare ya bila kufungana dhidi ya El Merreikh kwenye mchezo uliofanyika Sudan tarehe 6 Machi 2021.

Simba inaenda kukutana na Kaizer Chiefs hii leo ambayo ipo nafasi ya Tisa kwenye msimamo wa Ligi ya Afrika Kusini lakini ilimaliza nafasi ya pili kwenye kundi C, nyuma ya Wydad Casablanca.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!