BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limemuomba, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, awasamehe masheikh walioko mahabusu na gerezani, wakikabiliwa na tuhuma na makosa mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Ombi hilo limetolewa leo Ijumaa, tarehe 14 Mei 2021 na Katibu Mkuu Bakwata, Nuhu Nabir Mruma, wakati akitoa salamu za Bakwata, katika Baraza la Eid El-Fitr Kitaifa, lililofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mruma amesema, kwa kuwa masheikh hao wamekaa mahabusu na gerezani kwa muda mrefu, bila kujua hatma yao, baraza hilo linaomba waachwe huru au mamlaka zinazosimamia kesi hizo ziharakishe uchunguzi.
“Lakini kuna kesi za masheikh mbalimbali walioko gerezani, kwa muda mrefu kwa tuhuma za makosa mbalimbali, tunaomba mamlaka husika ziharakishe uchunguzi wa mashtaka au upelezi na kwa kuwa wamekaa muda mrefu gerezani bila kujua hatma yao, tunaomba wasamehe au wafutie mashtaka yao yote,” amesema Mruma.
Katibu Mkuu huyo wa Bakwata, ameshauri vyombo vinavyosimamia kesi kurahakisha uendeshaji wa kesi zilizokaa muda mrefu mahakamani, ili wahusika watendewe haki.
“Bakwata, inarudia kutoa maombi yake kwa serikali na vyombo vya kushughulikia haraka kesi za muda mrefu kwani hunyima haki wahusika na huipa serikali gharama,” amesema Mruma.
Miongoni mwa Masheikh walioko mahabusu kwa tuhuma mbalimbali ni Masheikh 23 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar wanaokabiliwa na Kesi ya Jinai Na. 121/2021, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Masheikh hao waliakamatwa mwaka 2012.
Tuliambiwa barakoa ni mbinu za mabeberu. Tukazikataa. Sasa tumezipokea. Je na chanjo ya Corona si tusipokee tu? Kuna ubaya gani? Mbona chanjo nyingine tumekuwa tukizutumia kwa miaka mingi nazo zinatoka nje? Twende wa wakati Twende na ushauri wa wataalamu