Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana 854 wa JKT watimliwa kwa uasi
Habari Mchanganyiko

Vijana 854 wa JKT watimliwa kwa uasi

Spread the love

 

VIJANA 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), waliokiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa madai ya kutaka kumuona Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, wametimuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Walikusudia kwenda kudai kuandikishwa jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo jana Jumamosi, tarehe 17 Aprili 2021, katika hafla ya kutunukiwa Kamisheni kwa Maafisa wapya 393 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na nchi rafiki.

Maofisa hao wamehitimu mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, mkoani Arusha (TMA) na nje ya nchi, ambao wote wametunukiwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi Tanzania

Kati ya Maafisa hao, Maafisa 143 wa JWTZ wamehitimu mafunzo ya 1 ya Shahada ya 1 ya Sayansi ya Kijeshi iliyoanzishwa kwa ushirikiano wa TMA na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Maafisa 233 wa JWTZ wamehitimu kozi ya mwaka mmoja na maafisa saba kutoka nchi rafiki za Eswatini na Kenya wamehitimu kozi ya mwaka mmoja.

Jenerali Mabeyo amesema, tarehe 8 April 2021, vijana vijana 854 kati ya 2,400 waliokuwa wameahidiwa kupewa ajira na Rais na waliokuwa wakijenga ofisi ya Ikulu, Chamwino “waliamua kugoma, kukataa kufanya kazi eneo jingine na kuandamana kumwona Rais, wakishinikiza kutaka kuandikishwa jeshini.”

Amesema, hata walipotakiwa kusitisha mgomo huo “hawakusikia, kitendo hiki hakikubaliki, kitendo hiki cha kugoma au kuandamana jeshini ni kosa la uasi na kwa sababu hiyo, JKT imesitisha mkataba wao wa kujitolea kuanzia tarehe 12 Aprili 2021, na tayari imewasafirisha kuwarejea makwao. ”

“Kimsingi, Jeshi la Kujenga Taifa, si sehemu ya ajira, bali ni sehemu ya kujifunza stadi za kazi, tunasikitika vijana wale walifanya kazi kubwa na walikaa Jeshi la Kujenga Taifa takribani miaka mitatu.”

“Kutokana na tukio hili, tunatafakari utaratibu mpya wa vijana wa kujitolea kwenda Jeshi la Kujenga Taifa,” alisema Jenerali Mabeyo.

Kati ya Maafisa waliotunukiwa, Maafisa 143 wa JWTZ wamehitimu mafunzo ya 1 ya Shahada ya 1 ya Sayansi ya Kijeshi iliyoanzishwa kwa ushirikiano wa TMA na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Maafisa 233 wa JWTZ wamehitimu kozi ya mwaka mmoja na Maafisa 7 kutoka Nchi rafiki za Eswatini na Kenya wamehitimu kozi ya mwaka mmoja.

Jenerali Mabeyo, amewataka maafisa hao wapya kuheshimu, kuthamini, kuzingatia na kutunza viapo vyao katika maisha yao yote kwani viapo hivyo ndivyo vinaunda sheria ya ulinzi.

Ameongeza kuwa pamoja na kufanya uchunguzi zaidi wa kwa nini walifanya hivyo Jeshi limeamua kutafakari upya mpango wa kuchukua vijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na JKT.

Katika hatua nyingine, Jenerali Venance Mabeyo amemshukuru Rais Samia kwa Serikali kutoa Sh.2 bilioni, zilizotumika kujenga uwanja wa maadhimisho ya Kitaifa uliopo Ikulu Chamwino ambao umetumika kwa mara ya kwanza katika utoaji wa Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi na ambao utatumika kwa matukio mengine mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Jenerali Mabeyo ameishukuru, Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa bega kwa bega na JWTZ na amemhakikishia Rais Samia kuwa jeshi lipo imara kulinda mipaka ya nchi, wananchi na rasilimali za Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!