Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Iundwe Tume ya Majaji ifanye uchunguzi – Zitto
Habari za Siasa

Iundwe Tume ya Majaji ifanye uchunguzi – Zitto

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

 

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuunda Tume ya Majaji, ili kuchunguza fedha ‘zilizolipwa’ na watuhumiwa waliokiri makosa ya uhujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Pia ameshauri, tume hiyo ipitie taarifa na fedha zilizochukuliwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kubadilisha fedha za kigeni.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumapili tarehe 11 Aprili 2021, wakati akiwasilisha uchambuzi wa chama hicho kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa 2019/2020.

Wito huo ametolewa baada ya ripoti hiyo kubaini, kiasi cha Sh. 51.521 Bil zilizokuwa katika akaunti ya fedha za Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hazikutumika kutokana na kukosekana kwa sheria na kanuni za matumizi yake.

“Katika hili, sisi tuna pendekezo mahsusi na tunalipeleka kwa Rais Samia, aunde Tume ya Majaji ili kupitia malalamiko ya watu wote ambao walilipishwa fedha na DPP kwa mtindo wa kukiri makosa na kuzilipa fedha hizo serikalini.

“Wote watakaobainika kuwa walionewa, warejeshewe fedha zao na rekodi zao za jinai ziondelewe, tunajua watu wengi tu walionewa, walibambikiwa kesi wakalipishwa. Watu tumetoa michango mingi katika kesi za watu ambao tunajua walionewa,” amedai Zitto.

Mbali na wito wa uundwaji wa tume hiyo, ametoa wito kwa CAG Charles Kichere, kukagua akaunti yenye fedha zilizowekwa na walio waliothumiwa kuhujumu.

“Kuna taarifa ambazo zinazagaa kwamba fedha hizi na baadhi ya fedha ‘hizo’ zilikuwa zinawekwa kwenye akaunti malaumu katika Benki ya TIB, lakini akaunti ile ina signatories (watia saini) ya watu binafsi, inaonekana kama akaunti ya serikali.

“Kwa hiyo ni muhimu CAG kufanya ukaguzi wa eneo hili, ili watu waweze kufahamu kwanza fedha zilizokusanywa maduka ya kigeni zilikuwa kiasi gani zilizoporwa na namna gani watu watarejeshewa fedha zao.”

Pia Zitto ameshauri Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kufuatia ubadhirifu wa Sh. 3.27 bilioni, uliotokea katika Bandari za Mwanza na Kigoma.

“Mamlaka ya Bandari Tanzania imetajwa kwa kiwango kikubwa katika ripoti hii ya CAG, ambapo vilibainika vitendo vya ubadhirifu katika Bandari za Mwanza na Kigoma vya thamani ya Sh. 3.27 bilioni ambazo ziliibiwa kutoka akaunti za Benki.

“Tunapendekeza kuwa Mamlaka za Uteuzi zivunje Bodi ya Bandari na kuiunda upya ili kuweza kuweka misingi ya uwajibikaji katika Shirika,” ameshauri Zitto.

Wakati huo huo, Zitto amemshauri CAG Kichere, afanye ukaguzi katika miradi mikubwa ya bandari ili kujua undani wake.

“Tunashauri CAG afanye ukaguzi maalumu wa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Mamlaka ya Bandari, ili kupata uhalisia wa ubadhirifu katika TPA. Wakati ukaguzi huo unafanyika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!