Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa COVID-19: Prof. Lipumba ‘watu wana hofu’
Habari za SiasaTangulizi

COVID-19: Prof. Lipumba ‘watu wana hofu’

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

 

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema, wataalamu na wanasayansi Tanzania wamekuwa na hofu ya kueleza hali halisi kuhusu maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam, leo tarehe 7 Machi 2021 amesema, serikali itumie wanasayansi kukabili virusi vya corona.

“Hasa kwenye magazeti ya nje, watu wanaomba kutotajwa majina yao kutokana na woga wa kuingia matatani.

“Watu wana hofu, wanamashaka, wanaogopa. Tuiondoe hii hofu. Madaktari na wanasayansi waweze kufanya utafiti bila woga,” amesema.

Prof. Lipumba ameishauri serikali kushirikiana na mataifa mengine duniani ili kupata chanjo hiyo.

“Tunatoa wito kwa serikali kufanya utaratibu kwa kuwatumia wataalamu wa afya kufanyia uchunguzi chanjo za corona, hatimaye majibu ya wataalamu na ndio yaongoze uamuzi juu ya kutumia chanjo hizo.

“Tushirikiane na taasisi za kimataifa, tutumie wataalamu na tuwasikilize,” amesema Prof. Lipumba.

Tayari viongozi mbalimbali wa kiroho wamewataka waumini wao kuchukua tahadhari dhidi ya corona.

Hata hivyo, serikali imesisitiza Watanzania kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na virusi hivyo.

Na kuwa, miongoni mwa hatua muhimu ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka.

2 Comments

  • Naomba wahusika wanielimisha
    Wasafiri wanaotoka nje ya nchi (wakiwemo watalii) wanapimwa Corona kwa garama ya dola 100. Je wakionekana wameambukizwa na virusi vya Corona ndege inawakubali? Kama la, je watabaki nchini na watapatiwa matibabu? Ufukizaji au madawa ya wazungu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!