May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanakijiji DRC wavamia mlima wa dhahabu

Spread the love

 

KANDA ya video inayoonesha wakazi wa Bukavu, Kivu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokraia ya Kongo (DRC), wakiokota vipande vya dhabau, imesambaa kwa kasi katika mtandao wa twitter. Inaripoti mitandao ya kimatifa…(endelea).

Kutokokana na kusambaa kwa video hiyo, Serikali ya DRC imetuma vikosi vyake vya usalama kwenye maeneo hayo ili kuimarisha usalama.

Video hiyo inawaonesha wananchi hao wakiparura na kuchimba mashimo madogo sehemu mbalimbali za mlima huo, huku wakiokota vipande vingi vya dhahabu.

Pia sehemu ya pili ya video hiyo inaonesha, baada ya kukusanywa kwa vipande hivyo, vinaosha kwenye karai.

Mlima huo uliovamiwa, upo kilomita 35 Kaskazini mwa Bukavu.

Taarifa zinaeleza, mlima huo una kati ya asilimia 60 hadi 90 ya dhahabu.

error: Content is protected !!