Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bandari ya Kigoma yaipiku Mwanza
Habari za SiasaTangulizi

Bandari ya Kigoma yaipiku Mwanza

Bandari ya Kigoma
Spread the love

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema, maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari ya Kigoma yameanza kuleta matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa shehena ya mizigo pamoja na mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa tarehe 5 Machi 2021, katika Bandari ya Kigoma, Mhandisi Kakoko alisema, shehena na mapato katika bandari hiyo yameongezeka kiasi cha kuipiku Bandari ya Mwanza ambayo ndiyo iliyokuwa ikiongoza kabla ya maboresho hayo.

Alisema, Bandari ya Kigoma ambayo inahusisha bandari zote zilizopo Ziwa Tanganyika, imeanza kufanyiwa maboresho kuanzia mwaka 2016/17, ikihusisha ujenzi wa magati, ununuzi wa mitambo, ujenzi wa maghala na majengo ya abiria pamoja na ujenzi wa ofisi za kisasa za makao makuu ya bandari hiyo ambazo ziko katika hatua za mwisho kukamilika.

Mkurugenzi huyo alisema, maboresho hayo, yalisukumwa na kasi kubwa ya ongezeko la mahitaji ikilinganishwa na miundombinu iliyokuwepo.

Alisema bandari za Ziwa Tanganyika zimekuwa kiungo kikubwa cha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za DRC, Burundi na Zambia, biashara kubwa ikiwa ni mazao yanayozalishwa Tanzania.

Kutokana na hali hiyo alisema, bandari hizo zimekuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa wananchi wa mikoa inayozunguka Ziwa Tanganyika kwani mazao yao yanapata wanunuzi wengi wanaovutiwa na maboresho ya bandari.

Alisema, bandari hizo pamoja na kuanza kazi kwa reli, kumesaidia kupunguza bei za bidhaa ambazo husababishwa na gharama kubwa za usafirishaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (PTA), Mhandisi Deusidedit Kakoko

Alisema bado kuna maboresho zaidi yanaendelea katika bandari Kuu ya Kigoma yanahusisha ujenzi wa gati ya maboti ya Kibirizi, gati ya abiria na makasha na ujenzi wa bandari Kavu ya Katosho.

“Tumekusudia kuifanya bandari ya Kibirizi na Kigoma kuwa ya mizigo ya nje na ile ya Katosho itakuwa ya ndani, ” alisema Kakoko.

Alisema matarijio ya kuongezeka zaidi kwa shehena na abiria ni makubwa kutokana na maboresho ya meli yanayotarajiwa kufanywa na Kampuni ya Huduma za Meli zikiwemo MV Mwongozo, MV Liemba na MT Sangara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!