Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko NBS yatangaza nafasi za kazi 300
Habari Mchanganyiko

NBS yatangaza nafasi za kazi 300

Spread the love

 

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetangaza nafasi za kazi za muda 300 kwa Watanzania ya kutenga maeneo kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tanzania, hufanya sense ya watu na makazi, kila baada ya miaka 10 na mara ya mwisho, ilifanyika mwaka 2012.

Taarifa iliyotolewa na kaimu mtakwimu mkuu wa serikali, ofisi ya NBS, tarehe 4 Machi 2021, inaeleza kwamba, muombaji awe tayari kufanya kazi sehemu na mazingira yoyote ndani ya Tanzania Bara.

Waombaji wanatakiwa kuwa ni Watanzania wenye; umri wa miaka 18 au zaidi, elimu ya kidato cha nne na kuendelea mwenye uzoefu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na NBS na elimu ya shahada/stashahada/astashahada ya urasimu ramani, upimaji wa ramani, mipango miji na kozi zinazofanana na hizo watapewa kipaumbele cha kwanza.

 

Taarifa hiyo inaeleza, mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 Machi 2021 saa 9:30 alasiri, “waombaji wote wanatakiwa kuambatisha vyeti vya taaluma na wasifu (CV). Watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili huo watajulishwa. Aidha, NBS haitahusika na gharama zozote za kuhudhuria kwenye usaili huo.”

4 Comments

  • Epimark Njau nipo tayari kushiriki ,shule ya misingi mkoani, secondari ujenzi secondari ,ndanda high school,

  • Thanks for this announcement and opportunity for all Tanzanians ,but I failed to apply this opportunity that has already expired

  • Kwa majina naitwa Godfrey ..kwa maelezo yaliotolewa apo nimeelewa na mimi ningehitajo niwe mmoja wapo katika hizo fursa Elimu yangu ni kidato cha nne

  • Kwa majina naitwa hawa saidi ningependa niwe mmoja wapo wa maombi yakazi elimu yangu ni kidato channe nina miyaka 23

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa vya ujenzi, samani kwa shule ya msingi Sinyaulime, Chuo cha FDC Morogoro

Spread the loveBENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya...

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

error: Content is protected !!