Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chanzo kifo cha Balozi Kijazi chatajwa
Habari za Siasa

Chanzo kifo cha Balozi Kijazi chatajwa

Spread the love

 

ALIYEKUWA Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania, Balozi John Kijazi (64), amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga…(endelea).

Chanzo hicho kimetajwa leo Jumamosi tarehe 20 Februari 2021, na Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais, Utumishi, Dk. Laurian Ndumbaro, wakati anasoma wasifu wa Balozi Kijazi.

Wasifu huo, umesomwa katika Ibada ya maziko ya mwili wake, iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu Augustino, Korogwe mkoani Tanga, kabla ya maziko, yanayofanyika nyumbani kwao, wilayani humo.

Balozi Kijazi, alifariki dunia saa 3:10 usiku, tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, jijini Dodoma alikokuwa anapatiwa matibabu.

Dk. Ndumaro amesema, Balozi Kijazi alilazwa hospitalini hapo baada ya kauugua kwa muda mfupi tarehe 1 Februari 2021.

“Balozi Kijazi ameugua kwa muda mfupi, ambapo tarehe 1 Februari 2021, alilazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma, hadi mauti yalipomkuta na amefariki kwa maradhi ya moyo,” amesema Dk. Ndumbaro.

Balozi Kijazi alizaliwa tarehe 18 Novemba 1956, akiwa moto wa pili katika familia ya watoto 10. Ameacha mke mmoja, Fransiscar Kijazi, na watoto watatu wa kiume, David, Emmanuel na Richard.

Naye Allan Kijazi, naibu katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii ambaye pia ni mdogo wake na Balozi John Kijazi amesema, kifo cha kaka yake kimetokana “kushindwa kufanya kazi kwa moyo.”

Allan ambaye pia ni Kamisha wa Uhifadhi wa Taifa (Tanapa), amesema, kifo hicho ni pigo kwa familia yao lakini yote ni mapenzi ya Mungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!