May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Padre Katoliki afariki dunia

Padre wa Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni, Jimbo Katoliki la Singida, Marehemu Parick Njiku

Spread the love

 

PADRE wa Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni, Jimbo Katoliki la Singida, Parick Njiku, amefariki dunia jana Ijumaa, tarehe 19 Februari 2021, katika Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma. . Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kifo hicho kimetangazwa na Mhashamu Baba Askofu, Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida.

“Mhashamu Baba Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida, anatangaza kifo cha Padre Patrick Njiku, aliyekuwa anafanya Utume wake katika Paroka ya Kristo Mfalme Kibaoni.”

“Kilichotokea tarehe 19 Februari 2021 katika Hospital ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma,” imesema taarifa ya Askofu Mapunda.

Taarifa ya Askofu Mapunda imesema, misa ya kuuaga na mwili wa marehemu Padri Njiku, itafanyika tarehe 23 Februari 2021, saa 1:00 asubuhi, katika Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni, alipokuwa anafanyia utume enzi za uhai wake.

error: Content is protected !!