Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba yawaonya wachezaji na viongozi, “hatuna tatizo na FCC”
Michezo

Simba yawaonya wachezaji na viongozi, “hatuna tatizo na FCC”

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again'
Spread the love

 

BODI ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba jijini Dar es Salaam, imetoa onyo kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo watakaokwenda kinyume na taratibu, watachukuliwa hatua pasina kuangalia ukubwa wa mtu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, imesema, mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo, unakwenda vizuri kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC).

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi mdogo wa mwenyekiti, unaofanyika leo Jumapili, tarehe 7 Februari 2021, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano ya Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wanaowania nafasi hiyo ni, Murtaza Mangungu na Juma Nkamia.

Ameanza kwa kumwombea radhi, Mwenyekiti wa Bodi, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa kutokufika kwenye mkutano huo kwani yuko nje ya Tanzania “kwa ajili ya Simba, akirudi tutaona.”

Try Again amesema, wamejipanga kuhakikisha wanatetea tena ubingwa wa ligi kuu na kufika mbali kwenye michuano ya Kbalu Bingwa Afrika.

Amesema, mwenyekiti wa bodi, “amesema, anataka kusimamia nidhamu ya wachezaji, menejimenti, viongozi. Hatutaangalia ukubwa wa mchezaji au kiongozi,” amesema

“Rai kwa wachezaji, kazi yao ni kucheza mpira, wafanye hivyo. Sisi tutahakikisha maslahi yao yanapatikana mapema,” amesema Try Again

Makamu huyo mwenyekiti, ametumia fursa hiyo, kuwaeleza wanachama kwamba, Simba imekuwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali za umma, ikiwemo Tume ya Ushindani Tanzania (FCC).

“Kumekuwa na maneno mengi, FCC siyo tatizo, FCC ni taasisi ya umma, inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na sisi kama Simba hatujakosea na niwahakikishe, jambo letu la mabadiliko, linakwenda kukamilika ndani ya siku chache zijazo,” amesema Try Again huku akishangiliwa na wanachama

Amewaomba wanachama hao, kumchangua kiongozi atakayeshirikiana na bodi kusonga mbele pasina kurudi nyuma.

“Tuleteeni kiongozi ambaye atakuja kwenda sambamba na utaratibu na mabadiliko. Hatutaki kurudi nyuma, tunataka kwenda mbele. Hatutaki tena kuja kufanya uchaguzi mdogo,” amesema Try Again.

1 Comment

  • Mechi ya leo wachezaji wameniboa sana kuanzia dk ya 58 wamecheza chini ya kiwango kiasi kwamba unaweza ukawapunguzia mshahara wamezembea sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!