May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea Simba aitumia Yanga kuomba kura

Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba

Spread the love

 

MGOMBEA wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema kuwa moja ya ajenda zake nyingine, akipewa ridhaa ya kuongoza atahakikisha anaifunga Yanga pindi wanapokutana nayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mgombea huyo ameyasema hayo hii leo 7 Februari 2021, kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam huku moja ya ajenda ikiwa ni uchaguzi mdogo.

Mangungu alipopata nafasi ya kunadi sera zake mbele ya wanachama wa klabu hiyo, amesema kama wakimpa ridhaa pamoja na mambo mengine lakini atahakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wao wowote watakaokutana na watani zao Yanga.

“Jambo moja wapo mkinipa ridhaa nitahakikisha Simba inashiriki michuano ya ndani na nje ya nchi na jambo la kwanza nitahakikisha tutaifunga Yanga,” alisema mgombea huyo.

Aidha mgombea huyo alisema, Simba kwa sasa inahitaji mawazo mapya ili iweze kusonga mbele na kueleza kuwa atatumia siku 60 kuhakikisha mchakato wa mabadiliko unakamilika.

“Simba mpya inahitaji mawazo mapya na mitazamo mipya ili iweze kusoka mbele, nitajitahidi kuongeza mapato ya klabu na nitahakikisha mchakato wa mabadiliko unakamilika ndani ya siku 60,” aliongeza Mangungu.

Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swedy Nkwabi aliyejihuzuru nyadhifa hiyo tarehe 14 Septemba, 2019.

Wagombea wanaowania kinyang’anyiro hiko ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Nchemba, Juma Nkamia pamoja na Murtaza Mangungu mbunge mstaafu wa jimbo la Kilwa Kaskazini.

error: Content is protected !!