Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC ‘yajitutumua’ kwa Marekani
Habari za Siasa

NEC ‘yajitutumua’ kwa Marekani

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Spread the love

TUME ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC), imeitaka serikali ya Marekani kueleza, ni  namna gani uchaguzi mkuu uliyopita nchini  Tanzania ulivyoingiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

 Akizungumza na gazeti moja la kila siku, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles amekana madai hayo na kusema, “hayo ni maoni yao, uchaguzi haukuwa na matatizo.”

Jaji Kaijage, alikuwa akijibu kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Michael Pompeo, kwamba serikali ya Washington, imeamuru kuwawekea vikwazo vya kuingia nchini humo, watu wote waliohusika  kuvuruga uchaguzi mkuu uliyopita nchini Tanzania.

Amesema, si vema kwa Marekani kueleza mambo kiujumla jumla. Wanapaswa kueleza ni kwa namna gani uchaguzi mkuu ulivurugwa ama kuingiliwa.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa uchaguzi mkuu ulihudhuriwa na waangalizi wa nje, na kwamba kama kungekuwa na tatizo lingejionesha kwenye ripoti zao.

Taarifa ya Marekani kuweka vikwanzo kwa baadhi ya maofisa wa Tanzania bila kutaja majina, iliwekwa hadharani tarehe 19 Januari 2021.

Michael Pompeo

Marekani kupitia kwa waziri wake huyo, imeeleza kuwa kabla ya wakati wa uchaguzi huo, kulikuwapo mlolongo wa matukio yanayohusu wagombea upinzani katika nafasi za ubunge na udiwani, kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha.

Amesema, mbali na madai hayo, kuliibuka pia vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwamo upinzani kukamatwa na polisi, kunyanyaswa na kuzimwa kwa mtandao wa mawasiliano – intaneti.

Unyanyasaji huo wa upinzani, ulisababisha mamia ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupita bila kupingwa, kabla ya hata ya uchaguzi wenyewe kufanyika.

Ripoti zinasema baadhi ya wagombea wa upinzani walikumbana na matukio ya kutekwa, kuvamiwa na wengine kuenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali.

Karibu vyama vyote vya upinzani vimekuwa vikitoa matamko ya kulaani na kukemea hali hiyo.

Kumekua na ripoti kuwa baadhi ya wagombea walioenguliwa kwenye mchakato huo walikosea kufuata vipengele kadhaa wakati wa ujazaji wa fomu zao za uteuzi.

Hata hivyo, baadhi ya makosa yaliyodaiwa kufanywa na wagombea wa upinzani na ambayo yaliwaondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, yalifanywa pia na baadhi ya wagombea wa CCM, lakini wale wa CCM wote waliruhusiwa kuendelea na uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!