Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wahamiaji 36 wa Ethiopia, Somalia wadakwa Dar
Habari Mchanganyiko

Wahamiaji 36 wa Ethiopia, Somalia wadakwa Dar

Spread the love

WAHAMIAJI haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini Tanzania kinyume na taratibu, wamekamatwa. Anaripoti Mwandishi Wetu

Wahamiaji hoa wamekamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 15 Novemba 2020 kwenye fukwe za Mbweni jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 18 Novemba 2020, Mkuu wa Mkoa huo (RC), Aboubakar Kunenge, ametoa onyo kali kwa raia wa Tanzania wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha ili wapate fedha.

Kunenge amesema, wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia tarehe 15 Novemba kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao 30 wanatoka Ethiopia na sita wanatoka Somalia.

Amesema, hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka sheria, haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.

Pia, mkuu huyo wa mkoa, amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Kwa upande wake, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi Edmund Mrosso, amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini kinyume na taratibu.

Aidha Kamishina Mroso amesema, kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao adhabu inaelekeza kifungo cha miaka 20, faini ya Sh.20 milioni au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!