Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Milioni 39 wapona corona duniani
Habari Mchanganyiko

Milioni 39 wapona corona duniani

Spread the love

MAAMBUKIZO ya virusi vya corona (COVID-19) duniani yamefikia milioni 56.1, waliopona milioni 39.1 na waliofariki kutokana na ugonjwa huo wakiwa milioni 1.3. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mtandao wa worldometer hadi leo jioni Jumatano tarehe 18 Novemba 2020 umeripoti, Marekani inaongoza kwa kuwa na maambukizo milioni 11.69 kati yao, milioni saba wamepona na waliofariki wakiwa 254,315.

India inafuatia nafasi ya pili ikiwa na maambukizo milioni 8.92, waliopona milioni 8.3 na waliofariki dunia kutokana na virusi hivyo wakiwa 131,114.

Taifa la Brazil linashika nafasi ya tatu likiwa na maambukizo milioni 5.9, kati ya hao waliopona milioni 5.3 na waliofariki dunia wakiwa 166,743.

China ambako ugonjwa huo unaelezwa ulianzia mwishoni mwa mwaka 2019, inashika nafasi ya 65 duniani ikiwa na maambukizo 86,369, kati ya hao, waliopona ni 81,411 na vifo vikiwa 4,634.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!