Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yawapitisha Ndugai, Dk. Tulia kuwania Uspika
Habari za Siasa

CCM yawapitisha Ndugai, Dk. Tulia kuwania Uspika

Job Ndugai
Spread the love

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeteua majina mawili ya wanachama wake, watakaogombea Uspika na Naibu Spika wa Bunge la 12 la Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, chama hicho, kimeteua jina moja la mwanachama wa chama hicho kuwania Uspika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Uteuzi huo umefanywa na kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokutana juzi Alhamisi jijini Dodoma tarehe 5 Novemba 2020 chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Walioteuliwa ni; Job Ndugai kuwa mgombea Uspika na Dk. Tulia Ackosn kugombea Naibu Spika wa Bunge  la Tanzania.

Katika Bunge la 11 lililomaliza muda wake, Ndugai ambaye ni mbunge mteule wa Kongwa alikuwa Spika huku Dk. Tulia ambaye naye ni mbunge mteule wa Mbeya Mjini alikuwa Naibu Spika.

Kupitishwa wao pekee ina maana, wanakwenda kutetea nafasi hizo huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kushinda kutokana na wingi wa wabunge wa CCM.

Pia, kikao hicho, kimemteua, Zubeir Ali Maulid kuwa mgombea Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Kama ilivyo kwa Ndugai na Dk. Tulia, naye Maulid alikuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi lililomaliza muda wake ambaye anakwenda kutetea nafasi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!