Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wateule waitwa Dodoma
Habari za Siasa

Wabunge wateule waitwa Dodoma

Steven Kigaigai, aliyekuwa Katibu wa Bunge
Spread the love

WABUNGE wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wametakiwa kufika Dodoma kwa ajili ya usajili unaoanza leo Jumamosi hadi tarehe 9 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kikao cha kwanza cha Bunge la 12, kitafanyika Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 7 Novemba 2020 ofisi za bungeni, Dodoma amesema, “kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge jipya kitafanyika tarehe 10 Novemba 2020.”

Amesema, usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika ofisi ya Bunge Dodoma.

bunge la tanzania

Kagaigai amesema, wabunge wateule wote wanapaswa kufika wakiwa na nyaraka; hati ya kuchaguliwa/kuteuliwa kuwa mbunge na nakala ya kitambulisho cha Taifa.

Pia, Kadi ya Benki yenye namba  ya akaunti ya mbunge; cheti cha ndoa kinachotambuliwa na Serikali (kwa wenye ndoa), cheti cha kuzaliwa cha watoto wenye umri chini ya miaka 18 (kwa wenye watoto), vyeti vya elimu/taaluma, nakala ya wasifu wa mbunge na picha (pasipoti size) nakala nane.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!