Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Sh. 7,000 kuziona Simba na Yanga
Michezo

Sh. 7,000 kuziona Simba na Yanga

Spread the love

BODI inayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza viingilio kwenye mchezo utakaowakutanisha Yanga dhidi ya Simba ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Tsh. 7,000 kwa upande wa mzunguko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo Yanga watakuwa mwenyeji unatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili ya tarehe 7 Novemba, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni.

Viingilio vingine kwenye mchezo huo vitakuwa Tsh. 30,000 kwa VIP A, Tsh. 20,000 VIP B, Tsh. 15,000 VIP C na Tsh. 10,000 kwa upande wa viti vya machungwa.

Mechi hiyo ambayo itavuta hisia za mashabiki na wapenzi wa mchezo wa soka nchini kutokana na timu zote kuwa na vikosi imara na kuleta ushindani mkubwa kwenye Ligi mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa raundi ya nane ambapo Yanga yupo mbele ya Simba kwa tofauti ya pointi sita.

Mpaka sasa Simba amepoteza michezo miwili kwenye ligi hiyo na kwenda sare mmoja katika michezo nane waliocheza huku Yanga ikiwa haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa ila ilikwenda sare dhidi ya Tanzania Prisons.

Huenda kwenye mchezo huo Simba watakosa huduma ya washambuliaji wake wawili, Meddy Kagere na Chriss Mugalu kutokana na kuumia sambamba na kiungo wao raia wa Brazil, Greson Fraga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!