Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu alia kutelekezwa
Habari za Siasa

Lissu alia kutelekezwa

Tundu Lissu
Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amelalamika kutelekezwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza na kwenye mkutano wa hadhara jijini humo tarehe 17 Oktoba 2020, Lissu amesema tofauti na mikoa mingine aliyokwenda kufanya kampeni, katika jiji hilo hawakupata msaada wowote kutoka kwa polisi.

Ametumia jukwa la kisiasa kumfikishia ujumbe Mkuu wa Jeshi la Polisi chini (IGP), Simon Sirro kwamba, Polisi Dodoma kuna tatizo.

“Katika Makao Makuu ya nchi yetu, tumeachwa hivi hivi na Jeshi la Polisi la mkoa huu, tunajihangaikia wenyewe barabarani.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema akivuka Ziwa Victoria kwa kutumia kutumia mtumbwi akieleka Ukelewe

“Yaani IGP (Simon Sirro) kama unanisikia, huna RPC (mkuu wa jeshi la polisi wa mkoa) hapa…., inakuwaje mgombea urais yeye ndiye anayeongoza msafara kwenye malori makubwa kama haya?

“Ni utendaji gani huu? Tumesindikizwa kila mahali na polisi isipokuwa hapa Makao Makuu ya nchi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!