Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu, Mbowe, Sheikh Ponda, Maalim Seif kumfuata Lowassa
Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Mbowe, Sheikh Ponda, Maalim Seif kumfuata Lowassa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

JIMBO la Monduli, Arusha lililokuwa likiongozwa na Edward Lowassa, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 2015, linatarajia kuwa na ugeni mzito leo Jumatatu tarehe 19 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Wageni hao ni Tundu Lissu, mgombea urais Tanzania kupitia Chadema; Sheikh Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania; Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Kampeni za Lissu, zimepata nguvu katika lala salamq za kampeni hizo ambazo zimesalia siku tisa kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Tundu Lissu, mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni ya Lissu, leo Jumatatu anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo matano, miongoni mwao ni Monduli ambalo mgombea wake ni Fredreck Lowaasa, mtoto wa Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Hata hivyo, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kumalizika, Lowassa aliyewahi kuwa mbunge wa Monduli alitangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbowe na Maalim Seif, wanatarajiwa kuongeza nguvu kwenye jukwa la Lissu na Sheikh Ponda kwenye kampeni za majimbo hayo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Jijini Arusha, Lissu na ‘kampani’ yake wanatarajia kushambulia jimbo hilo la Monduli kisha Arumeru na baadaye Longido. Pia wanatarajia kushambulia Jimbo la Hai ambapo Mbowe ndiyo mgombea wake Ubungo kisha atamalizia na Moshi Mjini.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!