Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Wanataka kuni – Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif: Wanataka kuni – Lissu

Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamadi, mgombea urais visiwani Zanzibar amesema, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inataka kumfungia kama Tundu Lissu, mgombea urais Tanzania kupitia Chadema alivyofungiwa kufanya kampeni kwa siku saba. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Ni baada ya Kamati ya Maadili ya ZEC kumtaka kufika mbele yake leo tarehe 15 Oktoba 2020 kujibu tuhuma zilizowasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini kwamba,  anashawishi wafuasi wake kupiga kura tarehe 27 Oktoba 2020 badala ya tarehe 28 Oktoba 2020.

“…nimetakiwa nifike Kamati ya Maadili ya ZEC. Eti nimelalamikiwa na Chama cha Demokrasia Makini kwa kuwaambia watu wakapige kura Oktoba 27.

Maalim Seif, M/kiti ACT-Wazalendo Taifa

‘Wanataka kuni-Lissu. Hawa wanatumika na CCM. Kama Mwinyi (Dk. Hussein Mwinyi, mgombea urais Zanzibar kupitia CCM) ana hoja akajibu jukwaani. Narudia sote tukapige kura Oktoba 27,” ameandika Maalim Seif.

Sheria ya Uchaguzi Zanzibar imeweka utaratibu kwa baadhi ya watumishi wa umma hasa wanaosimamia siku ya uchaguzi, kupiga kura siku moja kabla ya siku ya uchaguzi husika.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!