Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maharagande ajinadi kwa ahadi saba Segerea
Habari za Siasa

Maharagande ajinadi kwa ahadi saba Segerea

Mbarara Maharagande, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalumu ya Chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

MGOMBEA Ubunge Segerea jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Mbarala Maharagande, ametaja vipaumbele saba ambavyo atavitekeleza pindi atakapochaguliwa na kuwa mbunge. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Maharagande ametaja vipaumbele hivyo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 wakati anazungumzia ahadi zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Mgombea huyo amesema kipaumbele chake cha kwanza ni ushirikishaji wa wananchi kwenye upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

Amesema katika utekelezaji wa kipaumbele hicho, ataanzisha ofisi maalum itakayoratibu shughuli za mbunge na wananchi wa Segerea ambayo itawekwa utaratibu maalum wa kufikiwa na wananchi wote.

“Kwa kushirikiana na madiwani, nitaweka utaratibu wa kufanya vikao vya pamoja na Kamati za Maendeleo ya Kata mara kwa mara ili kuainisha masuala ya msingi kwa kila kata yanayotakiwa kusimamiwa na kufanyiwa kazi,” amesema Maharagande.

Pia, Magaragande ameahidi  kuanzisha Taasisi ya Wananchi wa Segerea (Segerea Foundation) itakayoendeshwa na mfuko wa maendeleo wa jimbo ambayo itawaunganisha pamoja wadau wa maendeleo wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi za vyama au dini.

Kipaumbele cha pili ni kuwasilisha changanoto za wananchi wa Segerea katika vikao vya maamuzi, pamoja na kusimamia utungwaji wa sheria rafiki kwa wananchi.

“Katika hili Nitafanya yafuatayo, kuwawakilisha vyema wakazi wa Segerea katika vikao vya Maamuzi. Kuishauri, kuikosoa na kuisimamia Serikali itekeleze wajibu wake kwa maslahi ya wananchi,” ameahidi Maharagande.

Maharagande amesema, kipaumbele cha tatu kitakuwa utatuzi wa changamoto za ajira kwa kuwakutanisha watoa ajira na watu wanaotafuta kazi.

“Tutaorodhesha wadau wote wenye kuweza kutoa fursa za ajira ikiwemo viwanda vilivyopo ndani ya Jimbo la Segerea na maeneo mengine. Tutashirikiana na vijana waliomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo kuona namna gani wanavyoweza kupata ajira rasmi na au kujiajiri,” amesema Maharagande.

Kipaumbele cha ni nne, kuboresha sekta ya elimu kwa kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu wanapata elimu. Pamoja na kujenga shule katika kata ambazo hazina shule.

“Katika sekta ya elimu tutashirikiana na mabaraza ya maendeleo kata na manispaa kuongeza vyumba vya madarasa, madawati, kuzitambua na kusaidiana na Wananchi walioanzisha shule za awali kupata vifaa vya kujifunzia na kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji maalumu,” amesema Maharagande.

Maharagande amesema “aidha, ujenzi wa shule mpya katika baadhi ya kata na kushirikiana na wadau wa sekta ya elimu jimbo kutatua changamoto zilizokuwepo. Masuala mengine juu ya elimu tutayafuatilia na kuyasimamia kutoka Serikali Kuu.”

“Nitaanzisha uratibu wa kampeni ya kuwapatia wananchi bima ya afya kwa kushirikiana na wadau. Utoaji wa elimu kuhusu masuala ya usafi wa mazingira na afya itafanyika. Suala la uzoaji wa takataka litaratibiwa vizuri. Tutahakikisha usafi wa mazingira unaboreshwa ili kuepuka maradhi mbalimbali,” ameahidi Maharagande.

Maharagande amesema, kipaumbele chake cha sita kitakuwa ni uboreshaji wa miundombinu hasa ukarabati wa barabara na mitaro ya maji taka kwa kutumia fedha za ndani na za wafadhili, pamoja na kuanzisha vituo vipya vya daladala.

“Nitafanya uboreshaji wa mitaro ya maji na kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la uharibifu unaotokana na mafuriko pembezoni mwa mto msimbazi. Suala la upatikanaji wa maji safi na salama ili kuepuka magonjwa kama UTI, na Uchimbaji wa visima katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa maji litafanyika. Ujenzi wa madaraja katika maeneo yanayokubwa na mafuriko kipindi cha mvua litasimamiwa,” ameahidi Maharagande.

Pia, Maharagande ameahidi kutatua tatizo la ukosefu wa maeneo ya kuzikia (makaburi) katika baadhi ya Kata.

Kipaumbele cha mwisho alichoahidi Maharagande ni uboreshaji sekta ya michezo na burudani kwa kuwasaidia upatikanaji wa vifaa vya michezo na maeneo yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!