Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi: Tunawashikilia maofisa watatu ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Polisi: Tunawashikilia maofisa watatu ACT-Wazalendo

Spread the love

POLISI Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, linawashikilia maofisa watatu wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo katika kituo cha polisi Osterbay. Anaripoti Regina Mkonde, Kinondoni … (endelea).

Maofisa hao wanaoshikiliwa ni; Dotto Rangimoto (Afisa Habari Msaidizi), Dahlia Majid (Afisa wa Uchaguzi) na Arodia Peter (Afisa Habari na Uenezi) ambao inadaiwa walikamatwa na polisi Ijumaa iliyopita tarehe 25 Septemba 2020.

Maofisa hao walikamatwa wakiwa ofisi za chama hicho zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 amesema, hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa kuwa liko chini ya Idara ya Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

“Wapo katika Kito cha Oysterbay, lakini hawajakamatwa na Polisi Kinondoni, kwa hiyo siwezi kuzungumzia. Wako chini ya makao makuu ya upelelezi ndio maafisa wake wamewakamata,” amesema Kamanda Taibu.

Awali, MwanaHALISI Online ilimtafuta Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, ambaye alijibu hana taarifa za kukamatwa kwa maafisa hao.

“Hizo taarifa ndio nazisikia kwako, sina taarifa za kwamba Jeshi la Polisi wamewakamata,” amesema Kamanda Mambosasa.

Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo amesema, mawakili wa chama hicho wanafuatilia kama maafisa hao watapewa dhamana au watafikishwa mahakamani kesho Jumatatu tarehe 28 Septemba 2020.

“Toka jana wamekataa kuwatoa tulitafuta wanasheria kushughulikia, sababu leo sio siku ya kazi labda kesho watapelekwa mahakani tuon,” amesema Rithe.

MwanaHALISI Online linaendelea kutafuta uongozi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu kwa habari zaidi kuhusu suala hili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!