Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe amwelezea Lissu anavyowachanganya CCM
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe amwelezea Lissu anavyowachanganya CCM

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema (katikati) akiwasili uwanja Ndege JK Nyerere. Kushoto Freeman Mbowe na John Mnyika (kulia).
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, Chadema amesema, mwitikio wa wananchi katika mikutano ya kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Tundu Lissu umewafanya viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchanganyikiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Hai … (endelea).

Mbowe ambaye ni Mgombea Ubunge Hai mkoani Kilimanjaro amesema hayo juzi Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020 wakati akihutubia kwenye mkutano wake wa kampeni wa kuomba wananchi wamchague.

Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema, Lissu anashinda katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

“Nina hakika Lissu anakwenda kushinda urais wa nchi hii kwa sababu mikoa yote, wilaya zote na kata zote CCM wamechanganyikiwa. Tunawaambia CCM wajiandae kuondoka,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema, Chadema kikifanikiwa kuunda Serikali yake, kitapeleka Muswada wa Sheria ya Maridhiano kwa ajili ya kuliunganisha Taifa.

“CCM wametufanyia mambo mabaya sana lakini tunakwenda kuikamata nchi baada. Kitu cha kwanza Chadema itafanya, tutapeleka mara moja Muswada wa Sheria ya Maridhiano na kuunda Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa kulipiza kisasi ili kuunganisha nguvu ya wananchi bila kujali ubaguzi wa vyama,” amesema  Mbowe.

Kwa upande wake, Lissu akihutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza juzi Ijumaa , aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura za mafuriko ili kumwezesha kushinda kwa kishindo.

“Mwanza… tarehe 28 Oktoba 2020 tukapige kura ya mafuriko kama haya ya leo, tukapige kura ya kibunga, mkipiga kidogo wataiba, tukiwashinda robo watatuhujumu, tukipiga kwa wingi hawawezi,” alisema Lissu

“Wazee kwa vijana, shangazi kwa wajomba na wote tukafanye hiki ambacho kitatuondoa katika utawala huu ambao unatutia umasikini, 28 Oktoba 2020 iwe tarehe ya kila mmoja kuifanya ya ukombozi,” alisema Lissu.

Lissu alisema “Tukapige kura ya kimbuga, ili askari wetu, mwalimu wetu, mkulima wetu, mfanyakazi wetu, mfabiashara, mama ntilie, machinga na tarehe 28 Oktoba ndiyo siku ya kuamua. Tukapige kura ya kutuondoa katika utawala huu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!