Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu 2020: Serikali haipaswi kufanya haya
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi Mkuu 2020: Serikali haipaswi kufanya haya

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imebainisha mambo matatu yasiyopaswa kufanywa na Serikali wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

 NEC imebainisha mambo hayo kupitia kitabu chake cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020.

Mambo hayo ni; vyombo vya ulinzi na usalama kutumia madaraka yao kukandamiza wagombea, wafuasi au chama chochote cha siasa.

Aidha, vyombo hivyo vitekeleze majukumu yake kwa weledi.

         Soma zaidi:-

Pili; kuingilia au kuzuia isivyo halali mikutano iliyoitishwa na vyama vya siasa au wagombea kwa mujibu wa ratiba za uchaguzi.

Tatu; kumhamisha mtumishi yeyote wa Serikali anayehusika na shughuli za uchaguzi mpaka mchakato wa uchaguzi ukamilike.

Endapo Serikali itaona kuna ulazima wa kumhamisha mtumishi kama huyo ni lazima ishauriane na NEC.

Endelea  kufuatilia MwanaHalisi Online, MwanaHalisi TV na mitandao yetu ya kijamii Facebook, Twitter na Instagram kwa habari na taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!