BENKI ya KCB imeingia mkataba wa mwaka mmoja na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ wenye thamani ya Tsh 500 Milioni kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa Habari, upande wa KCB Bank uliwakilishwa na Bali Chale kwa niaba ya Mkurugenzi wa benki hiyo, huku upande wa TFF uliwasilishwa na Stephen Mguto ambaye ni makamu wa Rais na Mwenyekiti wa bodi ya Ligi.
Katika tukio hilo Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Kcb Christina Manyenye alisema kuwa hii ni mara ya nne mfululuzo kwa Bank hiyo kutoa udhamini kwenye Ligi hiyo kwa kuwa wanaamini kuwa michezo ni sehemu ya ajira kwa vijana na wanawaunga mkono Tff katika kufanikisha malengo yao katika sekta ya mpira wa Miguu.
“Kwa kipindi kingine tumekaa hapa kusaini mkataba wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wanne mfululizo, sisi kama KCB Bank tumeona kwamba michezo ni sehemu ni moja ya mahali wanapoendeleza uchumi kwa kuwa tunaamini kuwa tunakuza ajira nchini.
“Tunawasapoti TFF ambao wanapigaja kuona vipaji vya wachezaji wetu vikue kwa hiyo tunawapa mkono pia waweze kufanya kazi nzuri wanaoifanya sasa hivi,” alisema Manyenye.
Stephen Mguto ambaye ni makamu wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa bodi ya Ligi alieleza kuwa wanapenda kuendelea na KCB katika kusapoti mpira wa Tanzania kwa kuwa waanamini hiki walichokitoa ni kikubwa.
“Yatosha kuwafahamisha kuwa tunaingia mwaka wanne kwa udhamini wa KCB na tunaamini kuwa wako hapa kuishi na sisi TFF na tunachukulia kuwa hiki wanachokitoa ni kikubwa kwa kuwa kinaongezea pale tulipopunguka,” alisema Mguto.
Udhamini wa benki hiyo utaongeza chachu kwa klabu za Ligi Kuu katika kujikwamua kuichumi kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji klabu katika shughuli za kila siku.
Ligi hiyo ilianza 6 Septemba, 2020 kwa msimu mpya wa 2020/21 ambapo mpaka sasa klabu zote zimeshacheza jumla ya michezo miwili na mingine kutalajia kuendelea mishoni mwa wiki hii.
Leave a comment