Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli nusura awatumbue DED, DC mkutanoni
Habari za Siasa

Magufuli nusura awatumbue DED, DC mkutanoni

Rais John Magufuli, mgomba Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM
Spread the love

JOHN Mwaipopo, Mkuu wa Wilaya ya Igunga (DC) na Revocatus Kuuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo (DED) mkoani Tabora, nusura watumbuliwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Igunga … (endelea).

Ni baada ya Rais John Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuagiza viongozi hao kuacha tofauti zao na kwamba, anajua vizuri mgogoro unaofukuta miongoni mwao.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni za urais za chama hicho leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020, wilayani Igunga mkoani humo.

“Ninafahamu hapa baadhi ya watendaji wangu nataka mjirekebishe, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya hapa, mimi napendaga kusema ukweli na msema ukweli mpenzi wa Mungu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ambaye ni ngombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, amemuagiza Kuuli kurudisha madeni anayodaiwa sambamba na kutatua changamoto za ardhi.

“Mkurugenzi aliko kule arudishe madeni yote anayodaiwa, atatue matatizo ya ardhi. Anachukua mpaka maeneo ya watu, hizi ndizo salamu zake mumpelekee,” amesema Rais Magufuli.

Rais huyo wa Tanzania amesema, wananchi wanapata mateso kutokana na kukosa watu wa kufikisha changamoto zao katika mamlaka husika.

“Mateso mengine mnayoyapata mlitakiwa mpate watu wa kuwasemea sababu hayafiki mahali inapotakiwa,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Rais Magufuli amesema mteule wake huyo aliwahi kumfukuza mwananchi aliyempelekea taarifa za kutishiwa usalama wa maisha yake badala ya kumsaidia.

“Kuna mtu mmoja alishinda kesi ya dhuruma zao kule baadae akawa anatishiwa kuuawa akaenda kwa mkuu wa wilaya kueleza alitishiwa kuuawa, mkuu wa wilaya akamfukuza baada ya siku mbili yule mtu akauawa, nasema uongoz ndugu zangu?” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!