Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maganja wa NCCR-Mageuzi ateuliwa kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Maganja wa NCCR-Mageuzi ateuliwa kugombea urais Tanzania

Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi kuwa mgombea urais wa Tanzania
Spread the love

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amemteua Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi kuwa mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, Jaji Kaijage amemteua Haji Ambar Khamisi kuwa mgombea mwenza. Maganja amekuwa mgombea wa sita kuteuliwa na NEC kugombea katika uchaguzi huo.

Jumla ya wagombea 17 walichukua fomu za uteuzi na mpaka sasa vimerudisha sita na wagombea wote wa vyama hivyo wameteuliwa na NEC.

Wengine waliokwisha teuliwa ni; John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea),  Mutamwega Mgaiwa wa (SAU) na Cecilia Mwanga wa Demokrasia Makini.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!