Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Uhondo wa EPL kuanza Septemba 12
Michezo

Uhondo wa EPL kuanza Septemba 12

Spread the love

LIGI Kuu ya Uingereza (EPL) msimu wa 2020/21 itaanza tarehe 12 Septemba 2020 ikishuhudia mechi sita zikipigwa katika viwanja tofauti. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ratiba ya ligi hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 20 Agosti, 2020 inaonyesha kuwa bingwa mtetezi wa ligi hiyo, Liverpool itaanzia nyumbani kuwakaribisha Leeds United waliopanda daraja.

Mechi za kwanza itakuwa Crystal Palace itakayoanzia ligi nyumbani kuwakaribisha Southampton. Fulham itacheza na mabingwa wa kombe la FA, Arsenal huku Tottenham Spurs ikiumana na Everton. West Brom itacheza na Leicester City na West Ham ikiwaalika Newcastle United.

Tarehe 14 Septemba 2020, itachezwa michezo miwili saa 2:00 usiku, Brighton itawakaribisha vijana wa Frank Lampad timu ya Chelsea na Sheffield Utd watacheza na Wolves.

Katika raundi hiyo ya kwanza, mechi mbili zimesogezwa mbele za Burnley dhidi ya Manchester Utd na Manchester City iliyokuwa icheze na Aston Villa.

Ligi hiyo itaendelea raundi ya pili tarehe 19 Septemba 2020 kwa timu zote 20 kushuka dimbani huku ikishuhudia mechi kubwa itakayozihusisha Chelsea itakayoikaribisha darajani timu ya Liverpool.

Mechi zingine siku hiyo ni Arsenal Vs West Ham, Aston Villa Vs Sheffield Utd, Everton Vs West Brom, Leeds Utd Vs Fulham, Leicester City Vs Burnley, Manchester Utd Vs Crystal Palace, Newcastle Utd Vs Brighton, Southampton Vs Spurs na Wolves Vs Manchester City.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!