Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Mkumbo atoa sababu kuwania ubunge Ubungo
Habari za Siasa

Profesa Mkumbo atoa sababu kuwania ubunge Ubungo

Kitila Mkumbo, mtia nia jimbo la Ubungo (Ccm)
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amechukua fomu ya kuomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpitishe kuwania ubunge Ubungo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Profesa Mkumbo amekabidhiwa fomu leo Jumatano tarehe 15 Julai 2020 katika ofisi ya wilaya ya Ubungo na Katibu wa CCM Wilaya yhiyo, Sylvester Yared.

Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo hilo ni Saed Kubenea wa Chadema ambaye hakuchukua fomu kuwania ubunge ndani ya chama hicho na haijafahamika kama atagombea kupitia chama kingine katika uchaguzi huo au la.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu, Profesa Mkumbo amezungumza na waandishi wa habari akisema ameanza mchakato wa kuwania ubunge kwa kuchukua fomu.

Alipoulizwa kwa nini anautaka ubunge wakati tayari yeye ni katibu mkuu wizara ya maji, Profesa Mkumbo amesema, “ni utumishi kwa umma, utumishi kwa wananchi, kwa hiyo ni nafasi nzuri ya kuwatumikia wananchi katika nafasi nyingine. Katibu mkuu ni ajira lakini suala la ubunge ni suala la uongozi ndiyo maana natafuta nafasi hii.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!