Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: R.I.P Mdhamini wa CCM ‘Lusinde’
Habari za Siasa

JPM: R.I.P Mdhamini wa CCM ‘Lusinde’

Balozi Job Lusinde
Spread the love

DAKTARI John Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesikitishwa na kifo cha Balozi Job Lusinde, aliyekuwa mdhamini wa chama hicho katika uasisi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Lusinde ambaye alikuwa miongoni mwa mawaziri 11 wa kwanza wa Serikali ya Tanganyika, amefariki dunia alfajiri ya tarehe 7 Julai 2020.

Leo tarehe 8 Julai na Rais John Magufuli, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameomb0leza kifo cha Balozi Lusinde, akisema kwamba atakumbuka mchango wake mkubwa alioutoa kwa taifa.

“Nimesikitishgwa na kifo cha Mzee wetu Balozi Job Lusinde. Nawapa pole familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa taifa akiwa waziri, balozi, mdhamini wa CCM na kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri,” ameombolewa Rais Magufuli.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, chama hicho kinamlilia Balozi Lusinde, kwa kuwa alikuwa sehemu ya waasisi wake.

“Chama kinamlilia Mzee wetu Job Lusinde, sehemu ya waasisi wetu, kiongozi katika chama na serikali, mzee na mshauri wetu wa chama kutoka Jiji la Dodoma.

“Mzee Lusinde alikuwa mjumbe wa Baraza la Wadhamini la CCM. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe,” ameandika Polepole katika ukurasa wake wa Twitter.

https://twitter.com/hpolepole/status/1280737889580650497?s=21

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!