October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilimanjaro: Majimbo 9, watia nia 124 CCM

Spread the love

IDADI ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika majimbo tisa mkoani Kilimanjaro, wanaotaka kuwa wabunge mpaka sasa imefika 124. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Kwa mujibu wa Jonathan Mabihya, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro ni kwamba, mpaka tarehe 6 Julai 2020, wanachama hao walikuwa tayari wamejitokeza kuonesha nia hiyo.

“Mpaka tarehe 6 Julai mwaka huu, tumepokea jumla ya wanachama 124. Ni wanachama ambao wanaoonesha nia ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo tisa ya mkoa huu,” amesema.

Majimbo tisa ya mkoa huo na idadi ya watia nia waliojitokeza kwenye mabano ni Rombo (14), Same Magharibi (13), Hai (8), Moshi Mjini (8), Moshi Vijijini (22), Same Mashariki (16), Siha (7), Mwanga (23) na Vunjo (13).

Mabihya amesema, matakwa ya Katiba ya chama hicho ni kuwa, wakurugenzi wa uchaguzi ni makatibu wa chama wa ngazi husika.

CCM imeeleza, wanachama walio na nia ya kuwania udiwani, uwakilishi na ubunge, wataanza kuchukua tarehe 14 – 17 Julai 2020.

error: Content is protected !!