Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ngono? Hakuna kitu hicho Chadema – Matiko
Habari za Siasa

Ngono? Hakuna kitu hicho Chadema – Matiko

Esther Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini
Spread the love

ESTHER Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini amesema, ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hakuna manyanyaso ya kingono. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Matiko ametoa kauli hiyo katika mahojiano yake na MwanaHALISI Online, kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono, zilizoibuliwa hivi karibuni na waliokuwa wabunge viti maalum wa chama hicho, dhidi ya viongozi wa Chadema.

Joyce Sokombi na Susan Masele, waliokuwa wabunge viti maalum kupitia Chadema, wakati wakitangaza kuhama chama hicho, walidai kwamba walikumbana na unyanyasaji wa kingono.

Sokombi na Masele walidai kwamba, wanawake wanaotaka nafasi za uongozi ndani ya Chadema, hulazimika kutoa rushwa ya ngono ili wapate wanachotaka.

Akizungumzia tuhuma hizo, Matiko ambaye aliwahi kuwa mbunge viti maalum kupitia Chadema, amesema hajawahi shuhudia mikasa ya unyanyasaji huo, tangu alipojiunga na chama hicho.

“Napata ukakasi sana nikisikia jamii inamhusisha mtu ukiteuliwa viti maalum unatumika kingono, huwa nasikitika sana. Wanasema mtu amepata sababu ya rushwa ya ngono. Mimi ni shuhuda mzuri sikuwa kupata unyanyasaji wa kingono. Sijawahi kuamini katika hilo sababu unashinda kwa sifa zako,” amesema Matiko.

Matiko amewahoji wanaodai kukumbana na unyanyasaji wa kingono, kwa nini hawakufichua mapema wanaohusika na unyanyasaji huo.

“Katika umri mimi ni mtu mzima. Ukisema unapata unyanyasaji inakua sio sahihi sababu mtu akikitongoza utamkatalia, na akienda mbali kwa kukubaka mimi kama mbunge lazima nitamchukulia hatua stahiki,” amesema Matiko.

Matiko amesema wanaotoa tuhuma hizo wanalengo la kuichafua taswira ya Chadema.

“Wameamua kuweka maneno kuichafua taswira sehemu waliyohama. Mimi siwezi sema unyanyasaji wa kingono upo. Unachaguliwa kwa sifa stahiki. Sitakaa niamini kama kuna vitendo hivyo,” amesema Matiko.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!