October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Kairuki awatangazia neema wawekezaji

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji, Angellah Kairuki

Spread the love

WAZIRI wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji, Angellah Kairuki amesema, serikali iko mbioni kukamilisha uhakiki wa madai ya ushuru wa asilimia 15 ya uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi unaodaiwa na kampuni mbalimbali ya uwekezaji nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 2, Julai 2020 wakati alipotembelea kuona shughuli za uzalishaji wa soda na maji katika kampuni ya vinywaji baridi jamii ya coca cola ya Bonite Bottlers iliyopo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

”Serikali inaendelea kufanya uhakiki wa kila madai yaliyowasilishwa tunajua ilikuwa ni muda mrefu lakini ambacho TRA na wizara ya fedha inafanya, inaendelea kurejesha na kutafuta suluhisho la kudumu ni mfumo gani zaidi wa kudumu ambao utafaa na utaweza kutumika,” amesema

”Najua wenye viwanda vya vinywaji watafurahia lakini utakuwa na tija na serikali itapata pia kile ambacho inastahili,” amesema Kairuki.

“Niwahakikishie ndugu zangu, serikali iko na nyie bega kwa bega na sasahivi inakamilisha uhakiki wa madai ya asilimia 15 ya uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi unaodaiwa na makampuni mbali mbali ya uwekezaji nchini na hata nyie Bonite,” amesema

“Niwapongeze bonite  kwa uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Sh.145 bilioni ambao mmewekeza niwaombe endeleeni kupanua  wigo wa uzalishaji katika wilaya na mikoa mingine na mbuni aina nyingine ya  uzalishaji wa bidhaa,”amesema Waziri Kairuki

Akisoma taarifa yake kwa Waziri Kairuki, Meneja  wa masoko  wa bonite  christopher Loiruki ameiomba serikali kuirejeshea kampuni hiyo Sh. 5.9bilioni  ambazo imekuwa ikiagiza sukari nje ya nchi toka mwaka 2016 kwa ajili ya kuzalishia soda.

error: Content is protected !!