Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto na wenzake waachiwa, asema…
Habari za Siasa

Zitto na wenzake waachiwa, asema…

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa chama cha siasa cha upinzania nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo na viongozi wengine waliokuwa wakishikiliwa na Polisi Mkoa wa Lindi wameachiwa kwa dhamana. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).

Zitto na viongozi hao walikamatwa jana Jumanne asubuhi tarehe 23 Juni 2020 wakiwa katika kikao cha ndani katika ukumbi wa Starnford Bridge, Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Wengine ni; Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara maarufu ‘Bwege’ , Akida Mawanja, Mlinzi wa Zitto na Shaweji Mketo ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni.

Pia, Swalehe Mketo aliyekuwa diwani wa CUF Kata ya Kibata, Abubakari Kama Mwenyekiti wa Jimbo Kilwa Kusini, Isihaka Mchinjika, Mwenyekiti wa Mkowa wa Lindi, na Mahadhi Mangona Katibu Mwenezi wa jimbo hilo.

Bonifancia Mapunda, wakiliwa kina Zitto amesema, uchunguzi wa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali haujakamilika na wametakiwa kuripoti kituoni hapo tarehe 1 Juni 2020.

Mara baada ya kuachiwa, Zitto amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi za  jimbo la Lindi Mjini ambapo amesema, kilichomtokea kinazidi kumuimarisha na wala hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya kutetea haki za wananchi na demokrasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!