ZITTO Kabwe, Kiongozi wa chama cha siasa cha upinzania nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo na viongozi wengine waliokuwa wakishikiliwa na Polisi Mkoa wa Lindi wameachiwa kwa dhamana. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).
Zitto na viongozi hao walikamatwa jana Jumanne asubuhi tarehe 23 Juni 2020 wakiwa katika kikao cha ndani katika ukumbi wa Starnford Bridge, Kilwa Masoko mkoani Lindi.
Wengine ni; Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara maarufu ‘Bwege’ , Akida Mawanja, Mlinzi wa Zitto na Shaweji Mketo ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni.
Pia, Swalehe Mketo aliyekuwa diwani wa CUF Kata ya Kibata, Abubakari Kama Mwenyekiti wa Jimbo Kilwa Kusini, Isihaka Mchinjika, Mwenyekiti wa Mkowa wa Lindi, na Mahadhi Mangona Katibu Mwenezi wa jimbo hilo.
Bonifancia Mapunda, wakiliwa kina Zitto amesema, uchunguzi wa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali haujakamilika na wametakiwa kuripoti kituoni hapo tarehe 1 Juni 2020.
Mara baada ya kuachiwa, Zitto amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi za jimbo la Lindi Mjini ambapo amesema, kilichomtokea kinazidi kumuimarisha na wala hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya kutetea haki za wananchi na demokrasia.
Leave a comment