Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wasaka urais CCM Z’bar wafika 22 
Habari za Siasa

Wasaka urais CCM Z’bar wafika 22 

Hussein Ibrahim Makungu, akichukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa 2020
Spread the love

MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaosaka kuteuliwa kugombea urasi visiwani Zanzibar, tangu chama hicho kifungue zoezi hilo tarehe 15 Juni 2020, wamefika 22. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Zoezi hilo ambalo linaenda sambamba na utafutaji wadhamini 250 kwa kila mgombea, linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 30 Juni 2020 saa 10:00 jioni.

Wakati upande wa Zanzibar wakijitokeza watia nia 22 mpaka leo tarehe 22 Juni 2020, upande wa Tanzania Bara hadi sasa amejitokeza kada mmoja tu, Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hussein Ibrahim Makungu, Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni, leo amekuwa kada wa 22 kuchukua fomu hiyo, katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, iliyoko Kisiwandui.

Makungu alitanguliwa na makada wengine watatu wa CCM, Mohamed Aboud Mohamed, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Bakari Rashid Bakar na Mhandisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, ambao wote wamechukua fomu hiyo leo.

Makada wengine wa CCM waliochukua fomu hiyo katika nyakati tofauti ni, Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Abeid Karume, mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanziba, Abeid Karume. Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Musa,  Dk. Hussein Ali Mwinyi, mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.

Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed Hijja Mohammed, Mohammed Jaffar Jumanne, Issa Suleiman Nassor, Mhandisi Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Maji. Mwatum Mussa Sultan, Haji Rashid Pandu, Abdulhalim Mohammed Ali.

Jecha Salum Jecha, aliyekuwa M wenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Dk. Khalid Salum Mohammed, Rashid Ali Juma, Khamis Mussa Omar, Mmanga Mjengo Mjawiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!