Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga wawajia juu mashabiki wao
Michezo

Yanga wawajia juu mashabiki wao

Mashabiki wa Yanga
Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Yanga umekemea vitendo vya mashabiki kuwazomea na kutokana wachezaji kiasi cha kuwakatisha tamaa na kuleta hali ya sintofahamu, licha ya klabu hiyo kupitia changamoto kadhaa kwa wakati huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga ambayo jana ililazimishwa sare na Azam FC, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na kuibuka hali ya jazba kwa upande wa mashabiki kutokana na kutovutiwa na viwango vilivyooneshwa na baadhi ya wachezaji kwenye mchezo huo.

Mashabiki wa klabu hiyo wameonekana kutupa lawama kwa washambuliaji wao David Molinga na Gnamien Yikpe kutokana na kutoonesha makali kwenye safu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imeeleza kuwa mashabiki wanapaswa kuisapoti timu yao pamoja na wachezaji ili kuleta mshikamano.

Gnamien Yikpe

Aidha katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Wakili Simon Patrick ilieleza kuwa, klabu hiyo kwa sasa inapitia changamoto ikiwamo kutopata matokeo mazuri na mashabiki kuumia, lakini kwa sasa ni muhimu kuleta ushirikiano.

Yanga ambayo kwa sasa imeshaanza mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo kwa kushilikiana La Liga pamoja na klabu ya Sevilla kutoka Hispania ambao wapo kama washauli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!