Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mfanyabiashara wa mafuta kizimbani Manyara
Habari Mchanganyiko

Mfanyabiashara wa mafuta kizimbani Manyara

Spread the love

SIMONI Lemeya Tukai, mfanyabiashara wa mafuta mkoani Manyara na wenzake watatu, wanatuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Hivyo, wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani humo. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Ezekiel Fabian Mayumba, aliyekuwa Afisa Afya na Mratibu wa Chanjo ya Mama na Mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro; Ally Sadick Mnkeni na Simaloi Baby Lemeya.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Manyara, Tukai ambaye ni mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Simon Lemeya pamoja na wenzake, watafikishwa katika mahakama hiyo baadaye leo tarehe 22 Juni 2020.

Katika taarifa yao iliyotolewa leo na Holle Makungu, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara, watuhumiwa hao wanadaiwa kughushi nyaraka na kufanya ubadhirifu wa fedha za Chanjo ya Kitaifa ya Rubella na Surua na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 5.6 milioni.

Taarifa hiyo ya Makungu imeeleza kuwa, watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani baada ya TAKUKURU kufanya uchunguzi na kubaini kwamba, mwaka 2014 walighushi saini za madereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ili kupata fedha hizo.

Tukai na wenzake wanakabiliwa na makosa ya matumizi ya nyaraka kudanganya mwajiri na ubadhirifu chini ya vifungu 22 na 28 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2017.

Makosa mengine ni kughushi na kusababishia hasara Serikali kiasi cha Sh. 5,609,00, kinyume cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

“ Ezekiel Fabian Mayumba aliandaa fomu za kutolea mafuta ambapo kwa kushirikiana na Simon Lemeya Tukai na Simaloy Baby Lemeya mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Simon Lemeya pamoja na Ally Sadick wa kituo cha Membi Filling Station, walighushi saini za madereva,” inaeleza taarifa ya Makungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!